TARI KIBAHA
Kituo Kidogo cha TARI Kibaha, kilichojulikana awali kama Taasis ya Utafiti wa Miwa (SRI) Kibaha, kilianzishwa mwaka 1971 chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kituo hiki kilifanya kazi kama Kituo cha Uzalishaji wa Mbegu za Miwa Afrika Mashariki, kutokana na ukaribu wake na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, jambo lililorahisisha uingizaji wa mbegu za miwa (germplasm), pamoja na hali nzuri ya hewa na ikolojia inayofaa kwa utoa maua kwa kiwango cha juu, ambacho ni muhimu kwa uzalishaji wa mbegu.
Mwaka 1989, programu ya utafiti wa mazao ya mizizi ilianza katika kituo hiki kama sehemu ya maeneo mengi ya utafiti (multi-locational site). Kuanzia mwaka 1994, kituo hiki kilipatiwa mamlaka ya kufanya utafiti wa mazao ya mizizi katika maeneo ya pwani yenye unyevunyevu na unyevunyevu wa wastani, pamoja na ukanda wa kati.
Aidha, mwaka 1990, kituo kilianzisha programu ya udhibiti wa hayawani hai (biological control) kufuatia uvamizi wa wadudu wa manjano wa muhogo (cassava mealybug) waliotoka katika nchi jirani.
Mnamo mwezi Julai 2018, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ilianzishwa rasmi, na ARI-Kibaha ikabadilishwa kuwa TARI–Kibaha, ikiwa na mamlaka ya kufanya, kuendeleza na kuratibu utafiti wa miwa nchini.