Fibre crops
Fibre crops
Mazao ya Nyuzi ni moja mazao yanayofanyiwa Utafiti na TARI, Utafiti huu unajikita katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuzi yenye ubora wa juu kwa kufanya utafiti wa mbinu bora za uzalishaji, mbinu za kisasa za kilimo, mbegu bora, na mikakati madhubuti ya kulinda mazao dhidi ya changamoto kama vile rutuba duni ya udongo na wadudu wa mazao. Utafiti huu unalenga kuzalisha mazao ya nyuzi yenye ustahimilivu na uzalishaji mkubwa kupitia mbinu kama vile utofauti wa mazao, usimamizi bora wa udongo, na matumizi ya mbinu za kisasa za uzalishaji. Mifano ya mazao ya nyuzi yanayolimwa Tanzania ni pamoja na pamba na mkonge.