Legumes
Legumes
Mazao ya mikunde ni moja ya mazao ambayo yanafanyiwa utafiti na TARI kwa lengo la kuboresha usalama wa chakula, lishe na kuongeza uzalishaji wa mazao haya, Utafiti wa kudhibiti wadudu na magonjwa, kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, na Utafiti wa urutubishaji wa udongo na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia mbinu kama utunzaji wa Nitrojeni (Nitrogen fixation). Utafiti huu unahusisha uzalishaji wa aina bora, agronomia, usimamizi wa baada ya mavuno, kuongeza thamani, lishe, na usimamizi wa Vina saba kwa mazao kama maharagwe ya kawaida, mbaazi, na kunde, na hatimaye kuchangia mifumo endelevu ya chakula na maisha bora ya watu.