Bidhaa Zetu
Bidhaa Zetu
Bidhaa za Tanzania Agricultural Research Institute (TARI) ni pamoja na mazao, mbegu bora, miche, na bidhaa zilizoongezwa thamani zinazotokana na tafiti za kilimo. Baadhi ya bidhaa hizo ni:
- Mbegu bora za mahindi kama T104, T105 na TH501
- Mbegu za mpunga aina ya SARO 5, Komboka, SATO1, na TARI RIC1
- Miche ya migomba inayozalishwa kwa teknolojia ya tissue culture
- Miche ya parachichi aina ya HASS, FUERTE, na nyingine
- Mizabibu na bidhaa za zabibu kama zabibu mbichi, zabibu kavu (raisins), na mvinyo
- Bidhaa za korosho kama korosho zilizokaangwa, korosho nyeupe, na divai ya matunda ya korosho
- Miche ya matunda na miti mbalimbali ya asili
- Vines za viazi lishe (OFSP)
TARI pia huzalisha na kusambaza teknolojia za kilimo kama:
- Teknolojia za kuongeza thamani ya mazao
- Teknolojia za kudhibiti wadudu na magonjwa
- Teknolojia za uhifadhi baada ya mavuno
- Kilimo himilivu kwa mabadiliko ya tabianchi