WADUDU WAHARIBIFU WA MAHARAGE NA JINSI YA KUDHIBITI
  • By MOSSES.BAYINGA
  • Leaflets
Publication Year : 2015

Author(s) : Kituo cha Utafiti wa Kilimo- TARI Selian

Maharage ni miongoni mwa mazao muhimu nchini Tanzania, yanatumika kama chakula kinachotowelea vyakula mbalimbali kama ugali, wali na makande. Aidha, majani yake yanaweza kutumiwa kama mboga za majani. katika miaka ya hivi karibuni, maharage yameanza kupata nafasi kama zao la biashara. Mbali na faida ya chakula, majani yaliyokauka ya maharage ni chanzo cha kipato kwa wakulima, kwani yanaweza kufungwa na kuuzwa kama chakula cha mifugo. Hata hivyo, wakulima wengi wanapata mavuno duni kutokana na changamoto mbalimbali, zikiwemo kutotumia mbegu bora, kutofuata mbinu sahihi za kilimo, kutokufahamu namna nzuri ya kudhibiti wadudu na magonjwa ya maharage. Kijarida hiki kina lengo la kuwaelimisha wakulima juu ya mbinu bora za kutmbua wadudu waharibifu ya maharage na jnsi ya kudhibiti ili kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao, kuboresha lishe na kuuza ziada kwa ajili ya kuongeza kipato cha mkulima na kuchangia katika uchumi wa Taifa kwa ujumla.