TUMIA MBEGU BORA ZA CHOROKO KUONGEZA TIJA NA KIPATO
  • By NICHOLAUS.SHOKELA
  • Leaflets
Publication Year : 2023

Author(s) : Tanzania Agricultural Research Institute (TARI)

Choroko ni zao jamii ya mikunde, ni zao la chakula na biashara. zao hili hustawi katika udongo aina tofauti usiotuamisha maji. Hustawi zaidi kwenye ukanda wa chini a wakati, yaani mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari.Choroko hukomaa kwa siku 60 hadi 75. Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamegundua mbegu mbalimbali kulingana na uhitaji na maeneo tofauti ya ekolojia ya kilimo.