Sunflower production and Post harvest Management
  • By NICHOLAUS.SHOKELA
  • Manuals
Publication Year : 2024

Author(s) : Taaisis ya Utafitifi wa Kilimo Tanzania(TARI)- Ilonga Centre

Alizeti ni zao muhimu la mafuta ambalo hutumiwa kutoa mafuta ya chakula na pia hutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine na mashudu yanatumika kwa ajili chakula cha mifugo. Zao hili hulimwa katika mikoa mingi hapa nchini kutokana na uwezo wake wa kuhimili hali ya hewa katika maeneo haya. Alizeti huzalishwa na wakulima wadogo na tija ndogo. Kwa wastani uzalishaji wa Alizeti ni tani 1 hadi 1.5 kwa hekta ukilinganisha na fursa ya kuzalisha tani 3 hadi 4 kwa hekta. Uzalishaji mdogo unachangiwa na matumizi madogo ya teknolojia bora ikiwa ni pamoja na matumizi madogo ya mbegu bora, mbolea, zana bora za kilimo, uwepo wa visumbufu na mabadiliko ya tabia nchi.